Jumatatu 2 Februari 2026 - 16:30
Mwaka 2026 umeshuhudia ongezeko la uungaji mkono kwa watu wa Palestina duniani

Hawza/ Tangia kuanza kwa mauaji ya halaiki yanayofanywa na Israel wamwagaji damu huko Ghaza, maandamano ya wananchi ya kuunga mkono taifa hili linalodhulumiwa yameendelea kote duniani, na waungaji mkono wa Palestina wamekuwa wakijitokeza mara kwa mara mitaani, katika viwanja na katika matukio ya umma.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, tangia kuanza kwa mauaji ya halaiki ya Israel wamwagaji damu huko Ghaza, maandamano ya wananchi ya kuunga mkono taifa hili linalodhulumiwa yameendelea kote duniani, na waungaji mkono wa Palestina wamekuwa wakijitokeza daima katika mitaa, viwanja na hafla za umma. Usiku wa Mwaka Mpya pia lilifanyika tukio jingine la kuonesha msimamo huu wa pamoja.

Bendera za Palestina zilionekana kwa wingi katika sherehe za nchi nyingi, na watu duniani waliunganisha nyakati zao za furaha na vitendo vya utu na ubinadamu. Jambo hili lenyewe limesababisha kutambulika zaidi kwa suala la Palestina na kuongezeka kwa ushiriki wa watu duniani kote katika kulishughulikia.

Huko Istanbul pia, Mjumuiko wa watu na Mapenzi ya Kitaifa, katika siku ya Mwaka Mpya, tarehe 1 Januari 2026, uliandaa maandamano makubwa ya kuunga mkono Palestina. Takribani watu 520,000, baada ya kukusanyika katika ua mkuu wa misikiti ya jiji hilo katika saa za alfajiri, walikusanyika kwenye Daraja la Galata na kupaza kauli mbiu za kuunga mkono Palestina.

Washiriki walisema kuwa maandamano hayo ni njia ya kuonysha mshikamano na Wapalestina wanaokabiliana na hali ngumu ya baridi kali ya majira ya baridi chini ya mzingiro mkali na mazingira magumu ya upinzani. Walisisitiza kuwa, ingawa hawawezi kuwa pamoja nao Ghaza na kushiriki nao mateso yao moja kwa moja, lakini kwa uwepo wao hapa wanaonesha mshikamano na uungaji wao mkono.

Chanzo: Palestinian Information Center

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha